April 18, 2016

MSHAMBULIAJI mkongwe wa Simba, Mussa Mgosi, ametangaza rasmi kuwa atastaafu kucheza soka la ushindani mwaka 2023.

Hiyo ni baada ya kuenea kwa taarifa za mkongwe huyo kustaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu akiwa Simba inayonolewa na Mganda, Jackson Mayanja.Mgosi alitua kuichezea timu hiyo msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Mtibwa Sugar.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgosi alisema ana miaka saba ya kucheza soka la ushindani kutokana na uwezo wake alionao wa kufunga mabao.


 “Muda wa mimi kuwa kocha au meneja bado aisee, ninahitaji kuendelea kucheza soka lenye ushindani, kama ni uwezo bado ninao, sioni sababu ya kustaafu soka.


“Hivyo kama Simba wakiona hawanihitaji, basi nitakwenda kwenye timu nyingine. Hakuna asiyejua uwezo wangu, lakini Simba nimeshindwa kuonyesha ushindani kutokana na majukumu niliyopewa na kocha (Mayanja) ya kuwa mchezaji ndani ya wakati mmoja nikiwa mshauri wake,” alisema Mgosi.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV