April 20, 2016

WAKATI timu yake ikifanya mazoezi kwa siku mbili mfululizo, beki wa kulia wa Simba, Hassan Kessy hajaonekana kikosini huku akielezwa kuvimba usoni baada ya kupigwa ngumi na Kipa Vincent Angban.
Angban raia wa Ivory Coast alimpiga ngumi Kessy baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba ilifungwa bao 1-0. 

Kessy

Kipa huyo alimpiga ngumi Kessy kwa kile kilichodaiwa kuihujumu timu hiyo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya, Edward Christopher.


Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, beki huyo hakutokea kwenye mazoezi ya juzi Jumatatu na jana Jumanne.Chanzo hicho kilisema, beki huyo mara baada ya mechi na Toto alisikika akitamka mechi yake hiyo ndiyo ya mwisho kwake kucheza akiwa na Simba, hivyo hatarejea kikosini tena.


 “Baada ya tukio hilo, alitamka kuwa hatarejea tena kwenye timu hiyo, hivyo uwezekano wa kuonekana mazoezini ni mdogo,”kilisema chanzo hicho.


Alipotafutwa meneja wa mchezaji huyo, Athumani Tippo kuzungumzia hilo alisema: “Kessy amepata uvimbe usoni baada ya kupigwa ngumi na Angban ndiyo maana hajajiunga na wenzake mazoezini kwani ana maumivu makali.”

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV