April 20, 2016

Kiungo wa Simba, Jonas Mkude amesema kama timu yake isipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ataondoka klabu ili akachezee timu nyingine msimu ujao.

Mkude aliliambia Championi Jumatano kuwa, ndoto yake kubwa ni kushiriki michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ngazi ya klabu na si vinginevyo.


Nafasi pekee ya Simba kushiriki michuano hiyo ambayo ni Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho Afrika, ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwani tayari imetolewa kwenye Kombe la FA.


Bingwa wa Kombe la FA ndiye anayeshiriki Kombe la Shirikisho Afrika hivyo Simba sasa imebakiwa na nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwakani.


 “Natamani sana msimu ujao tushiriki michuano ya kimataifa lakini mambo naanza kuyaona kama yanataka kuwa magumu, tusipokuwa makini hata hii nafasi iliyobaki tutaikosa.


“Endapo tutakosa nafasi hiyo, mimi nitaondoka zangu nikatafute maisha sehemu nyingine ambako naweza kutimiza ndoto zangu hizo,” alisema Mkude ambaye mkataba wake na Simba unamalizika Desemba, mwaka huu.


SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. UKIONA HIVYO KUNA FUKUTO KALI SANA SIMBA,KWA NINI MCHEZAJI ANASEMA ANA WASIWASI HATA UBINGWA KAMA WATACHUKUA,ETI MAMBO MAGUMU?MBONA WAKO KWENYE NAFASI NZURI BADO?HAKUNA NIDHAMU SIMBA KATI YA WACHEZAJI KWA WACHEZAJI NA HATA VIONGOZI KWA WACHEZAJI.KIONGOZI UNAPOSEMA ETI KAMA MTU ANATAKA KUONDOKA AONDOKE TU SIMBA KAIKUTA NA ATAICHA,HII MAANA YAKE NINI?UBINGWA MTAUSIKIA TU KAMWE KAMUUPATI MSIPOANGALIA.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV