April 14, 2016


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye Ligi Kuu Bara.

Simba iliondolewa katika hatua ya robo fainali baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Wagosi wa Kaya Coastal Union.

Mayanja amesema: “Kweli tumepoteza na halikuwa tunalolikusudia, sasa baada ya hapo tunapambana.

“Tukiendelea kuwaza au kulalamika, nafikiri itakuwa tunapoteza muda wa kufikiria mapambano yaliyo mbele yetu,” alisema.

Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 57.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV