April 20, 2025


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Simba wamepata ushindi mwembamba kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa nyumbani.

 Simba SC imekamilisha dakika 90 za mwanzo Uwanja wa Amaan kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.


Bao pekee la uongozi limefungwa na Jean Ahoua kwa pigo la faulo dakika ya 45 akitumia mguu wake wa kulia.

Mchezo wakukamilisha dakika 90 ugenini Simba wanakazi kutafuta ushindi mwingine ikiwa wataruhusu kufungwa bao kwa kuwa walitengeneza nafasi zaidi ya tano wakatumia moja.

Ahoua alikosa nafasi mbili za wazi akiwa ndani ya 18 dakika ya 49 kwa pigo la kichwa baada yakupigiwa krosi na Steven Mukwala na dakika ya 90 akiwa ndani ya 18 baada ya kupigiwa pasi na Mpanzu.

Kwenye eneo la kiungo Simba bado haijawa imara huku wapinzani wao Stellenbosch FC wakionekana kuwa na nguvu zaidi kwenye kujilinda.

Kibarua kizito kwa Simba ugenini kulinda bao ambalo wamepata nyumbani jambo ambalo linakwenda kuwa mtihani mgumu kwao ndani ya dakika 90 za kupata mshindi atakayetinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.


Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic