April 25, 2016


Baada ya Yanga kupangiwa na timu ya Sagrada Esperanca kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, uongozi wa timu hiyo umetamka kuwa, watafia uwanjani dhidi ya Waangola hao kwa ajili ya kuweza kupata mamilioni ya fedha ambayo waliyakosa baada ya kutolewa na Al Ahly kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imetua kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Waarabu Al Ahly kwa  jumla ya mabao 3-2 ambapo timu hizo zinatarajia kukutana kati ya Mei 6-8 jijini Dar na kurudiana wiki moja na nusu baadaye.

Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali, alisema kuwa kutokana na kuzikosa fedha ambazo waliahidiwa na uongozi wa timu hiyo kama wataitoa Al Ahly, wamepandisha hasira ya kuwatoa Waangola hao ili kuweza kufidia.

Hata hivyo, Pondamali hakuwa tayari kuweka wazi ni kiasi gani ambacho waliahidiwa kama wataitoa Al Ahly.

 “Yaani sasa tuna hasira mbili na hawa Esperanca, kwanza ya kutaka kuwafunga twende mbele kwenye michuano hiyo lakini nyingine ni kupata fedha ambazo tumeahidiwa kama kifuta jasho, sasa ukiunganisha mambo hayo mawili, tunazidi kuwatamani wapinzani wetu hao.

“Unajua kuwa kwenye mchezo ule dhidi ya Al Ahly, tuliambiwa na viongozi kuwa endapo tutawafunga basi tungeogelea mamilioni lakini tukashindwa kufanya hivyo, sasa zile fedha zimeletwa huku ambapo kwa zamu hii ni lazima tupigane kufa na kupona kwa ajili ya kuweza kuzipata,” alisema Pondamali.


2 COMMENTS:

  1. MNAWEZA,NI SWALA LA KUJIPANGA NA KUONYESHA NIDHAMU KAMA MLIOONYESHA KWENYE MCHEZO WA AL AHLY.

    ReplyDelete
  2. Mtafute wachezaji wenye miili kama Aguero hata ukiwa mfupi unaweza mikiki pia defensi iwe na wantu wenye kimo cha kutosha kupambana na krosi .

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV