Timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager jioni ya leo ilialikwa chakula cha jioni na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania iliyopo jijini Kampala.
Katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, wenyeji wakiwemo maofisa wa ubalozi , watanzania waishio nchini Uganda waliwapongeza wachezaji, viongozi kwa mchezo mzuri dhidi ya Uganda na kuwatakia kila la kheri katika safari ya jumatatu ya kurejea jijini Dar es salaam.
Stats inatarajiwa kuwasili Dar es salaam uwanja wa Mwl. JK Nyerere jumatatu saa 10 kamili jioni kwa shirika la ndege la Rwanda.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment