Sare ya mabao 2-2 kati ya Azam FC dhidi ya Yanga imeifanya Simba kupata nguvu kwamba lolote linawezekana.
Yanga na Azam FC jana zilipambana vilivyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lakini matokeo ya mwisho yalikuwa ni 2-2.
Azam FC ndiyo zinazoshika nafasi ya kwanza na ya pili, huku Simba ikiwa katiaka nafasi tatu.
Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja amesema inawezekana kabisa kuzifikia Yanga na Azam FC.
“Lakini lazima tupambane kweli, tuweke nguvu pamoja na kuaminiana. Kwa hali ilivyo hakuna kinachoshindikana,” alisema.
Simba inashuka leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kuwakaribisha Mbeya City kutoka Nyanda za Juu Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment