April 20, 2016

KIKOSI cha Simba, wikiendi hii kinatarajia kwenda Visiwani Zanzibar kujiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar Mei Mosi mwaka huu.

Simba inayonolewa na Mganda, Jackson Mayanja kwa kipindi kirefu imekuwa na desturi ya kukimbilia visiwani humo inapokabiliwa na michezo migumu , ikumbukwe kwenye michezo dhidi ya Yanga.

 Meneja wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa kikosi hicho kitaenda ‘camp’ hiyo kikiwa na lengo la kwenda kusaka muarobaini wa kuchukua pointi tatu watapokutana na Azam.


“Wikiendi hii tunaenda Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi yetu ya muda mfupi kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuvaana na Azam ambapo tunaamini kuwa kambi hiyo itatusaidia kuvuna pointi mbele ya wapinzani wetu,” alisema Abbas.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV