April 20, 2016

Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Issa Hayatou amemtumia salamu za pongezi Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) mwishoni mwa juma lililomalizika.

Katika salamu zake, Hayatou amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya Utendaji na yeye binafsi wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).


CAF wanaimani na uzoefu wa Ravia katika uongozi, kuwa ataendeleza uongozi bora kwa faida ya maendeleo ya soka visiwani Zanzibar.

Aidha, Hayatou amewatumia pia salamu za pongezi, Mzee Zam Ali na Ali Mohamed kwa kuchgauliwa kuwa makamu wapya wa Rais wa ZFA.

Hayatou amewatakia mafanikio mema katika nafasi mpya hizo walizochaguliwa na kuahidi CAF itaendelea kuwapa ushirikiano wa maendeleo ya mpira wa miguu visiwani Zanzibar.

ISSA HAYATOU

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV