April 19, 2016

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri timu za Azam FC na Yanga SC katika michezo yao ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).

TFF imezitaka Azam FC na Yanga kupambana katika michezo yao ugenini ili kupata matokeo mazuri yatakayozifanya ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, ikiwa kwa sasa ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa.




Azam FC inayoshirki michuano ya Kombe la Shirkisho barani Afrika (CAF CC), leo saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki inashuka Uwanja wa Olymique, Rades jijini Tunis kuwakabili wenyeji Esperance ST katika mchezo wa marudiano.

Straika wa Azam FC, Kipre Tchetche ataukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa majeruhi.

Kesho Jumatano, Yanga SC watakuwa ugenini kuwakabili wenyeji Al Ahly SC katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL), mchezo utakaochezwa saa 12:30 jioni katika uwanja wa Borg El Arab kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic