May 27, 2016

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI NA MKURUGENZI WA AZAM MEDIA, RHYS TORRINGTON WAKISAINI MKATABA, LEO.
Kampuni ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo wameingia mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni mbili wa kuonyesha matangazo ya moja kwa moja ya mechi za Ligi Kuu ya Wanawake na Ligi ya Taifa ya Vijana kwa timu za chini ya miaka 20.

Mkataba huo ni wa miaka mitano ambapo katika ligi ya wanawake, timu kumi ndizo zitakazoanzisha ligi hiyo huku ile ya U-20 itazishirikisha timu zote za vijana za Ligi Kuu Bara.


Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amesema katika malengo waliyojiwekea hapo awali ya kuinua soka hapa nchini, wanaona yanazidi kutimia kwani kitendo cha kuwepo kwa ligi kuu ya wanawake kunaashirikia kwamba itakuja kupatikana timu nzuri ya taifa ya wanawake.

“Tunayofuraha kubwa ya kusaini mkataba huu, tunaamini ligi hizo zitainua soka la nchi hii na kutimiza malengo yetu tuliyojiwekea hapo awali.


“Tunajua kuna timu nyingi za wanawake hapa jijini Dar, lakini nitoe angalizo tu kwamba hii ligi ni ya Tanzania kwa jumla, hivyo tutaangalia namna ya kupata timu kutoka mikoani na siyo kuegemea Dar es Salaam pekee,” alisema Malinzi.
Katika Ligi ya U-20, Malinzi alisema mfumo utakaoutumika ni ule wa kuwa na timu za umri huo kwa timu zote za Ligi Kuu Bara na endapo itatokea haitakuwa nayo, basi wataikata pointi tatu kwenye wa ligi kuu.

Naye Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, amesema dhumuni lao ni kuhakikisha wanalitangaza soka la Tanzania ndani na nje ya mipaka yake, na wataendelea kushirikiana na TFF katika kutimiza hilo.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic