May 27, 2016


Mashabiki wa Yanga sasa wana amani tele baada ya kupata uhakika kuwa kiungo kinda, Juma Mahadhi ni mali yao.

Awali ilionekana kama ni tetesi na taarifa zisizokuwa na uhakika sana. Lakini baada ya gazeti la michezo la Championi kutoa kwa mara ya kwanza, picha ya Mahadhi akisaini Yanga, mashabiki wengi wametuma maoni yao kwenye salehjembe@gmail.com na kusema, sasa wana uhakika na hawana hofu hata kidogo na uongozi wao.

“Utaona ni uongozi unaofanya mambo kwa uhakika, ligi inaisha wenyewe wameishamaliza kazi,” alisema Abdallah Hamis.

“Mimi nimefurahishwa kwa kuwa ninaamini wachezaji hao ni mapendekezo ya kocha,” aliandika Mchaki Salum.

“Mtazamo wangu ni tofauti kidogo, nimevutwa zaidi na kwamba Yanga imesajili wachezaji wote vijana na wenye vipaji, mtihani utabaki kwao na kwetu mashabiki kuwaunga mkono,” aliandika Stanley Mkomwa.


Mashabiki hao kila mtu alikuwa na maoni yake, wengine wakiwaasa wachezaji hao kubadilika na kujituma zaidi kwa kuwa Yanga ni sehemu yenye ushindani wa juu zaidi kuliko Simba na Coastal Union.

Yanga imewanaza Kessy kutoka Simba ambaye mkataba wake ulikuwa umeisha na Mahadhi kutoka Coastal Union iliyoporomoka hadi daraja la kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV