May 11, 2016


Beki kiraka wa Simba, Abdi Banda, amesema amefurahi kurejea katika kikosi cha timu yake lakini anaumizwa na kitendo cha kuwekwa benchi kwani anashindwa kudhihirisha kiwango chake.

Banda ambaye alisimamishwa na Simba kwa utovu wa nidhamu, mapema wiki iliyopita alijiunga kikosini na wenzake kwa ajili ya kuendelea na michezo ya Ligi Kuu Bara.

Banda amesema anafurahi kurudi kikosini wakati bado ligi inaendelea, lakini ameumizwa na kitendo cha kocha wake Jackson Mayanja kutomtumia dhidi ya Mwadui FC, wikiendi iliyopita.

Banda alisema kama angepewa nafasi katika mchezo huo, anaamini angeisaidia timu yake hiyo kuepuka kipigo cha bao 1-0 walichokipata.


“Kocha ananiweka jukwaani sijui kwa nini wakati nipo fiti kabisa kucheza, uwezo wa kucheza ninao na sijui kwa nini sikupangwa kwenye mechi dhidi ya Mwadui, basi hata kwenye benchi ningekuwepo, lakini cha kushangaza nakaa jukwaani,” alisema Banda.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV