July 7, 2021

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Didier Gomes leo kimesepa na pointi tatu mazima mbele ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.



Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma KMC 0-2 Simba na kuwafanya mabingwa hao watetezi kuibuka wababe.

Inakuwa ni mara ya pili kwa msimu huu kwa Simba kusepa na pointi tatu mbele ya KMC kwa kuwa mchezo wa kwanza walishinda bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.

Jumla Simba imesepa na pointi sita msimu huu mbele ya KMC.

Ni mabao ya Chris Mugalu dk ya 2 na 44 yalitosha kuipa pointi tatu Simba ambayo ilitoka kupoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.


KMC ilishuhudia mabao yote kipindi cha kwanza jambo lililowafanya kipindi cha pili kuongeza umakini kwa kuwa hawakuruhusu bao.


Beki wao Andrew Vincent alitolewa kipindi cha pili kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.


Sasa Simba inafikisha pointi 76 ikiwa na uhakika wa kutwaa ubingwa wao kwa kuwa pointi hizo zinaweza kufikiwa na Yanga ila tatizo itakuwa katika idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Simba imefunga jumla ya mabao 71 huku Yanga ikiwa imefunga jumla ya mabao 50 imecheza mechi 32 na imebakiza mechi mbili wakati Simba imecheza mechi 31 na imebakiza mechi tatu.

KMC inabaki nafasi ya sita na pointi 42 baada ya kucheza jumla ya mechi 32 ndani ya ligi.

9 COMMENTS:

  1. Ili Yanga waupate ubingwa, itabidi Mnyama afungwe mechi zake zote mbili bila ya kupata hata goli moja na ilizobaki na Matopolo wafunge mechi zao mbili zilizobakia na wapate mabao 19 kutu ambacho mustahili na chakuchekesha qanasema bbado hawajajakata tamaaaa. Hahahaaa

    ReplyDelete
  2. Simba bado ana mechi 3, ya coadtal, azam na namungo. Yanga bado mbili

    ReplyDelete
  3. FYi,
    Tusijisahaulishe Ili Simba ajihakikishie kuchukua kombe, ni lazima Morrison ashinde kesi yake CAS vinginevyo kombe watalisikilizia tu

    ReplyDelete
  4. Toto pia African Sports tawi la utopolo

    ReplyDelete
  5. Kesi gani hiyo isiyoisha, wewe bado unaamini propoganda za utopolo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic