Saa chache baada ya Ivo Mapunda kusaini Simba, kocha
wa Gor Mahia amesema amesikitishwa na uamuzi wa kipa huyo.
Bobby Williamson amesema hakuzungumza na Mapunda
kuhusiana na suala hilo.
“Ningeweza kumshauri zaidi, ni kipa mzuri na
nilikuwa namhitaji. Najua siwezi kumzuia lakini ningemshauri,” alisema.
“Nimesikitika, sisi tulitarajia kuzungumza naye mara
tu baada ya michuano ya Chalenji, lakini hakuna namna sasa. Zaidi namtakia mafanikio mema,” alisema kocha
huyo.
| IVO AKIWA MAZOEZINI GOR MAHIA... |
Ivo tayari amemwaga wino kuichezea Simba akitokea
Gor Mahia ambayo alichangia kuipa ubingwa msimu uliopita ingawa zaidi alikuwa
kipa namna mbili.
SALEHJEMBE ilikuwa blogu ya kwanza kuandika
kuhusiana na mafanikio makubwa ya Ivo nchini Kenya.
Moja ya gumzo ni taulo yake ambayo ilipata umaarufu
mkubwa na hasa kutokana na uwezo wake wa kupangua mikwaju ya penalty.







0 COMMENTS:
Post a Comment