May 2, 2016


KIMWAGA (KATIKATI) AKISHANGILIA PAMOJA NA KESSY NA MAJABVI...
Kiungo wa Azam FC aliyekuwa anaichezea Simba kwa mkopo, Joseph Kimwaga, amesema kuwa kwa sasa hafikirii kurudi kuichezea timu hiyo na badala yake anapiga hesabu ya kuhamia kwenye moja ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

Nyota huyo, alijiunga na Simba kwenye usajili wa msimu huu wa ligi kuu akitokea Azam FC iliyomtoa kwa mkopo kwa ajili ya kukuza kiwango chake baada ya kutoka kwenye majeraha.

Mshambuliaji huyo, tangu Februari, mwaka huu, ametoweka kwenye timu hiyo inayofundishwa na Mganda, Jackson Mayanja.

Kimwaga alisema amepoteza malengo yake yote aliyoyaweka ikiwemo kuichezea Taifa Stars mara baada ya kutua kuichezea Simba.

“Ujue kipindi nimepona nikitokea kwenye majeraha, Simba wenyewe ndiyo walinifuata Azam na kunitaka kwa mkopo kwa sharti la mimi kucheza ili kulinda kiwango changu kisishuke.

“Uongozi wa Azam ukakubali kwa baadhi ya masharti, likiwemo hilo la mimi kucheza katika kikosi cha kwanza, lakini cha kushangaza hilo sharti wamelivunja, hivyo nikaona niondoke zangu na kuwaachia Simba yao huku mimi nikijifua kivyangu.

“Nimepanga kutorejea tena kwenye timu hiyo na badala yake nitaangalia maisha kwingine kwa maana sitarudi tena Simba, kikubwa ninataka kwenda kwenye timu nitakayocheza kwa amani bila ya manenomaneno,” alisema Kimwaga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV