Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.
Hii ni mara ya pili Wambura kuula, lakini si rahisi Caf kumteua bila ya kupata pendekezo la jina kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF, atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.
Kuendelea kuchaguliwa kwa Wambura, pia kunamsaidia kuendelea kusomeka kwenye ramani ya soka na huenda kukamsaidia kurejea na kuwania tena uongozi wa Simba ambako kumekuwa na taarifa huenda akafikiria kufanya hivyo kwa mara nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment