May 26, 2016


Karibuni waandishi habari na wadau wengine kuilaki timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inayotarajiwa kutua leo Mei 26, 2016 saa 1.15 jioni baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).

Serengeti Boys haikuwahi kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano hiyo baada ya kutoka sare mechi tatu na kushinda mmoja kabla ya kuingia hatua ya kucheza mshindi wa tatu ambako ilishinda mabao 3-0 jana dhidi ya Malaysia.

India kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic