May 14, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Tambwe nafasi nzuri kabisa ya kuandika bao la tatu na la 22 kwake, lakini anapaishaa juuu
SUB Dk 86 Niyonzima anatoka nafasi yake Mbuyu Twite
Dk 83 Yanga wanazidi kushambulia kwa kasi wakionekana wanataka kupata kombe wakiwa na ushindi na Ndanda wanaonekana wanataka kutibua sherehe
GOOOOOO DK 79 Dk Salum Minely anaipatia Ndanda bao safi la kusawazisha
SUB 74 Yanga wanamtoa Ngoma na nafasi yake anachukua Matheo Simon

Dk 73, Mwashiuya anaonyesha mchezo usio wa kiungwana kabisa kwa kucheza rafu mbaya, lakini mwamuzi anaonekana hakuona
Dk 67 hadi 71, Ndanda wanaonekana kumiliki mpira muda mwingi lakini hawafanyi mashambulizi makali
DK 66, Raphael anaachia dhuti kali kabisa lakini kidogo linatoka nje ya lango la Yanga
Dk 63, Kamusoko anapata nafasi nzuri kabisa akiwa karibu kabisa na lango la Ndanda
Dk 59, Mponda anaachia shuti kali sana, lakini linapita juu kidogo

Dk 54 hadi 57, Yanga inamiliki mpira zaidi ingawa hakuna shambulizi kali
DK 53, Mwashiuya anatoa pasi nzuri kabisa kwa Tambwe akiwa katika eneo zuri, lakini anashindwa kufunga
KADI Dk 49 Sibo analambwa kadi ya njano kwa kufanya madhambi
Dk 47, Chove anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira wa adhabu wa Joshua
SUB Dk 46 Oscar Joshua anaingia kuchukua nafasi ya Mwinyi

MAPUMZIKODAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 42 hadi 45, kidogo kukanyagana kwa hapa na pale kunaanza kuonekana lakini Yanga wanaonekana kumiliki mpira zaidi
GOOOOOO Dk 41, Ngoma anaindikia Yanga bao safi baada ya kuunganisha krosi ya Mwinyi
Dk 38, Tambwe anapiga shuti kali, hatari hapa lakini linatoka kidogo nje ya lango la Ndanda
GOOOOOO Dk 35, Msuva anamalizia vizuri kabisa krosi ya Mwashiuya na kuandika bao la kusawazisha kwa Yanga, lakini ni la tisa kwake msimu huu
KADI Dk 32, Mponda naye analambwa kadi ya njano, haijajulikana nini kimetokea
KADI Dk 31, Yondani analambwa kadi ya njano kwa kumkwatua Mponda 


 GOOOOOOO Dk 28 Omary Mponda anaiandikia Ndanda bao la kwanza kwa mkwaju mzuri wa penalt
Dk 27, penaaaaaaaaat, Atupele anaangushwa hapa na Juma Abdul na mwamuzi anasema hii ni penalt
KADI Dk 25 Kiggi analambwa kadi ya njano kwa kuruka na kumtwanga Ngoma kipepsi
Dk 22, nafasi nyingine kwa Yanga, Tambwe anaachia kiki kali kweli, goal kick
Dk 21, Kamusoko anageuka na kupiga shuti kali la kushtukiza, lakini Chove anaonyesha umahiri wake, anadaka vizuri kabisa
Dk 19, Dida anafanya kazi ya ziada hapa, anaruka na kuokoa krosi safi ya Baruan Rashid wa Ndanda
Dk 17, Yanga wanafanya shambulizi zuri kabisa, krosi nzuri ya Niyonzima, Ngoma anapiga kichwa safi lakini sentimeta chache tu

Dk 14, Mwinyi anapiga krosi lakini Sibo anaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini inaonekana haina madhara kwa Yanga
Dk 12, Yanga wanapoteza nafasi nyingine baada ya Msuva kupiga shuti kuubwaaa wakati angeweza kutoa pasi kwa Tambwe aliyekuwa katika nafasi nzuri zaidi
Dk 10, Atupele anajaribu kupiga mpira wa juu baada ya kumuona Dida alikuwa ametoka mbele ya lango, lakini mpira unapita juu zaidi
Dk 7, Mwashiuya anamtoka beki wa kulia wa Ndanda, anaingia vizuri kabisa lakini kipa Jackson Chove anatoka na kuuwahi vizuri kabisa

Dk 5, Dida analazimika kuruka juu kuuwahi mpira usimfikie Atupele Green aliyekuwa akijaribu kuuwahi
Dk 4, Ngoma anawatoka mabeki wawili na kumpa pasi nzuri Niyonzima lakini anashindwa kulenga lango
DK 2, krosi safi ya Juma Abdul, hatari kabisa lakini Tambwe anaonekana hakuwa amejiandaa na kupiga juu, goal kick
Dk 1, mechi inaanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Ndanda lakini wanaonekana wako makini.


1-Deo Munishi Dida 
2-Juma Abdul 
3-Haji Mwinyi 
4-Vicent Bossou 
5-Kelvin Yondani 
6-Thaban Kamusoko 
7-Saimon Msuva 
8-Haruna Niyonzima 
9-Amis Tambwe 
10-Donald Ngoma 
11-Godfrey Mwashiuya 

BENCHI
-Ally Mustafa Barthez 
-Oscar Joshua 
-Mbuyu Twite 
-Pato Ngonyani 
-Salum Telela 
-Anthony Mateo 

-Paul Nonga

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV