May 1, 2016

KIKOSI CHA AZAM FC KILICHOCHEZA NA SIMBA MZUNGUKO WA KWANZA

MPIRA UMEKWISHAAAAAAAA

-Mgosi anaingia kuchukua nafasi ya Ugando, lakini hata hajagusa mpira
-KADI analambwa Mcha kwa kumlalamikia mwamuzi
-Bolou anapiga mpira wa adhabu lakini Agbani anaudaka kwaumahiri wa juu kabisa

DAKIKA 4+ ZA NYONGEZA
Dk 89, Mudathir anachambua vizuri kabisa na kupiga shuti kali, Agbani anaonyesha umahiri kwa mara nyingine kwa kupangua kwa ufundi wa juu kabisa
Dk 87, Majegwa anapoteza nafasi nzuri kwa Simba, badala ya kutoa krosi, anampa mikononi kipa Manula
Dk 86, Tchetche anajaribu shuti lakini Agbani anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 84, Nimubona anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliokuwa unakwenda langoni mwake na kuwa wa kurushwa
Dk 80, nafasi nyingine Simba wanapoteza kwa papara baada ya beki wake Nimubona kupiga shuti kuuubwa wakati angeweza kutuliza na kutoa pasi ndani

DK 79 Azam wanapata kona, inachongwa na Mcha lakini inakuwa ni moja ya kona zisizo na madhara ambazo Azam FC walipiga
Dk 78, Awadhi Juma anaweka vizuri mpira, akiwa katika nafasi nzuri anaachia shuti kuuuuubwaaa
SUB Dk 76, Azam FC wanamtoa Mugiraneza na nafasi yake inachukuliwa na Bolou Tchetche
Dk 75 bado Mugiraneza na Agbani wako wanatibiwa
SUB Dk 73, Simba wanamtoa Juuko na nafasi yake inachukuliwa na Brian Majegwa
Dk 71, Mudathiri anaachia shuti kali lakini Agbani anadaka kwa umahiri mkubwa.

Dk 70, Bocco tena, anawapiga chenga mabeki watatu wa Simba, anapiga shuti safi kabisa, Agbani anapangia
Dk 67 Bocco tena, yeye na kipa wa Simba, anauchop mpira lakini unatoka nje kidogo
Dk 66, Nimubona anaokoa shuti la Bocco lililokuwa linajaa wavuni. Kona, inachongwa lakini haina lolote
Dk 60, kazi nyingine nzuri ya Manula anapangua mpira unakuwa kona, inachongwa lakini ni butu
Dk 52 hadi 55 zinaibuka vurugu  baada ya Kiiza kumpiga teke Sure Boy naye naye akamkanyaka akiwa pale chini

Dk 52, Manula anafanya maajabu yake tena, anapangua faulo maridadi kabisa Tshabalala na kuwa kona ambayo haina madhara kwa Azam
SUB Dk 51, Hijja Ugando anaingia kuchukua nafasi ya Lyanga aliyeumia
Dk 46, Bocco anajaribu lakini kwa mara nyingine Agbani anakuwa makini
Dk 46, Azam FC wanaanza kwa kasi zaidi lakini Simba wanaonekana wako makini na hilo
SUB Dk 46, Mudathiri anaingia kuchukua nafasi ya Singano 'Messi' ambaye hakuonekana kabisa kipindi cha kwanza

&&&&&&&&&&&
MAPUMZIKO
DAKIKA 2+ ZA NYONGEZA
Dk 45, Mwalyanzi anapoteza nafasi nzuri kabisa akiwa karibu na lango la Azam, lakini anabutua tuuuu
Dk 42 hadu 45, kidogo mpira inaonekana kupunguza kasi na  mashambulizi makubwa
Dk 42, Manula anafanya kazi nyingine ya ziada na kudaka mpira kichwani mwa Kiiza
Dk 41, MWantika anafanya kosa, Kiiza anauwahi lakini Manula anakuwa na spidi zaidi anaokoa unakuwa wa kurushwa
KADI Dk 36, Aggrey analambwa kadi ya njano kwa kumrukia kwa makusudi Kiiza

Dk 33, Mwamuzi Akrama anamuonya kwa maneno nahodha wa Simba Jonas Mkude kwa kumwangusha Kipre
KADI Dk 29 Mwalyanzi anamwangusha Aggrey Morris, mwamuzi Mathew Akrama anamfuata akitaka kumpa kadi ya njano, lakini anagundua amesahau. Analazimika kwenda kuifuata kwa mwamuzi msaidizi, anarudi katika dakika ya 30 na kumlamba Mwalyanzi kadi hiyo ya njano
Dk 28 imetimia, Simba ndiyo zaidi wanamiliki mpira na zaidi ni katikati ya uwanja. Washambuliaji wake na viungo kama Mwalyanzi na Lyanga wanaonekana hawako makini kama utalinganisha na wale wa Azam FC wanaoonekana wana njaa ya mabao

Dk 25 sasa, Simba wamepiga kama pasi 28 hivi lakini mwisho wameishia kwa shuti dhaifu la Awadhi Juma
Dk 22, MWantika analazimika kulala na kuutoa mpira usimfikie Mwalyanzi, inakuwa kona. Inapigwa lakini haina faida kwa Simba
Dk 21 sasa, Azam FC ndiyo wamefika langoni mwa Simba mara nyingi zaidi. Lakini hawako makini katika umaliziaji
DK 19, Mwantika anafanya kosa kubwa, Kiiza anauiba mpira lakini kipa Manula anauwahi na kurekebisha kosa hilo

Dk 12 hadi 15, kiungo Sure Boy wa Azam FC anaonekana kuwa na mwendo mzuri na kuifanya Azam FC kutawala mchezo zaidi hasa katikati
Dk 11, nafasi nyingine kwa Azam FC lakini Bocco tena anapiga kichwa dhaifu kama kile cha kwanza
Dk 8, Azam FC wanaendelea kushambulia, Bocco anapokea krosi safi lakini anapiga kichwa fyongo
Dk 7, Mcha anabaki yeye na kipa Agbani wa Simba, lakini anampa mikononi mwake
Dk 2, Lyanga amapiga shuti Manula anapangua na kuwa kona, inachongwa Kiiza anapiga kichwa lakini Manula anapangua tena

Dk 1 mechi imeanza taratibu huku kila timu ikionekana iko makini na Azam FC inacheza zaidi katika eneo lake, Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Azam FC lakini ni goal kick.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV