May 17, 2016

Serengeti Boys wameonyesha wanaweza kweli baada ya kuwaonyesha soka wenyeji India kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mechi ya michuano ya vijana ya AIFF inayoendelea mjini Goa.

Boys walioonyesha soka safi ndiyo walikuwa wa safi walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Maziku Amani katika dakika ya 20.

Maziku tena aliunganisha mpira na kuandika bao la pili katika dakika ya 28 na kuwaduwaza wenyeji.

Baadaye India walionekana kuamka na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 36 kupitia Komal Thatal na hadi mapumziko ikawa 2-1.

Kipindi cha pili, vijana hao wa Tanzania ndiyo walionyesha soka bomba zaidi na kufanikiwa kupata bao jingine katika dakika ya 47, mfungaji akiwa Asad Ali.


Baada ya hapo, Boys walionekana kuuchezea zaidi mpira, wakipiga pasi za uhakika na kuwakatisha tamaa kabisa wenyeji hao ambao wana kikosi chao kilichotengenezwa chini ya uangalizi bora kwa zaidi ya miaka mitano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV