May 17, 2016


Juuko Murishid na Hamisi Kiiza watachukuliwa hatua kali baada ya kamati ya utendaji kukutana.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kamati hiyo itakutana na kuwaita ili wajieleze.


"Wakati tunajiandaa mechi na Majimaji tukijiandaa na safari ya Songea wachezaji Kiiza (Hamis). Juuko (Murshid), Nimuboma (Emiry) waliwashinikiza wachezaji wenzao wa kimataifa Angban (Vincent) na Majabvi (Justuce) kwenda kwenye mechi hiyo hadi watakapolipwa mshahara ambao baadaye wao walikwenda.

Kiongozi huyo wa juu wa Simba, aliweka msisitizo kwamba wanachosisitiza ni suala la nidhamu na hawatatoa nafasi kwa wachezaji kugeuka sehemu ya uharibifu wa utulivu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV