May 26, 2016


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema wazi kwamba halitaandaa michuano ya Kagame 2016.

TFF imesema kuwa suala la uandaaji wa michuano hiyo lilikuwa chini ya Zanzibar ambayo baadaye ilitangaza kujiondoa.

“TFF haikuwahi kusema itandaa michuano hiyo, ilikuwa chini ya Zanzibar ambayo imetangaza kujitoa. Maana yake mwanachama yoyote wa Cecafa anaweza kuingia na kusaidia.

“TFF iko katika wakati mgumu, moja ya timu, Yanga inashiriki michuano ya kimataifa na itacheza mechi mbili kwa mwezi, hakika itakuwa vigumu,” ilieleza sehemu ya kauli ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi.


Baada ya Zanzibar kujitoa dakika za mwisho, Cecafa ilitaka TFF kuingilia kati ya kuokoa jahazi kuhusiana na mashindano hayo ambayo kadiri siku zinavyosonga mbele, yamekuwa yakizidi kuyumba na huenda yanaweza kupotea siku moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV