May 2, 2016Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumanne Mei 3, 2016 saa 5:00 asubuhi itatangaza uamuzi wa rufaa nane zilizowasilishwa na kujadiliwa za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016.

 Kamati hiyo itatangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Jumla ya rufaa nane zinazohusu timu, kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo kwa Jumapili Mei mosi, 2016 kwenye ofisi za TFF jijini.

Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:
1.   Timu ya Geita Gold
2.   Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
3.   Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold
4.   Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
5.   Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
6.   Timu ya Soka ya Polisi Tabora
7.   JKT Oljoro Fc ya Arusha

8.   Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV