May 6, 2016

KIKOSI CHA ESPERANCA WAKATI KIKIWASILI KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE (JNIA) JIJINI DAR ES SALAAM, JANA USIKU.

Kocha Msaidizi wa Esperanca, Frank Moniz amesema wamesafiri hadi jijini Dar es Salaam kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kabla ya mechi yao ya pili dhidi ya Yanga nchini mwao.

Esparanca ya Angola, kesho inaivaa Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tayari timu hiyo ipo jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini jana usiku na ndege ya kukodi.

Moniz raia wa Angola amesema anaamini wana kila sababu ya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri hapa Tanzania.

“Ukifanya vizuri hapa, maana yake unaweka mazingira mazuri baadaye nyumbani.

“Tunataka kucheza vizuri huku na kuondoa presha kabisa. Tunajua Yanga ni timu nzuri lakini sisi tuna kikosi bora,” alisema.


Esparanca wanatarajia kufanya mazoezi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa, leo kabla ya kuwavaa Yanga kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV