May 28, 2016


Tamasha hilo limekata utepe leo Mei 28 na litafika tamati Juni 4, mwaka huu na linaganyika kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea, Ruvuma.

Washindi walikuwepo wengi lakini kwa upande wa wanaume, kinara alikuwa Hamad Rashid aliyetumia dakika 16:59, nafasi ya pili Ferdinand Haule aliyetumia dakika 18:22 wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Nathan Mpangala aliyetumia dakika 29:19 ambaye mbali na ushiriki huo, pia ni balozi wa tamasha.

Katika mbio za Km 21, John Mahagula aliibuka kinara kwa kutumia muda wa saa 1:32: 14, Jackson Faustine nafasi ya pili saa 1:41:17 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na  Abdallah Oscar aliyetumia muda wa saa 1: 50:48.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV