June 23, 2016
Achana na zile hadithi za kufikiria, sasa ni rasmi leseni ya mshambuliaji Obey Chirwa imetua katika ofisi za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Caf).

Leseni ya Mzambia huyo kutoka FC Platinums ya Zimbabwe, maana yake, Chirwa ruksa kuanza kuitumikia Yanga na ataanza kucheza katika mechi ya Jumanne dhidi ya TP Mazembe.

Mmoja wa maofisa wa Caf, ameiambia SALEHJEMBE kutoka Cairo, Misri kwamba kila kitu kimekamilika.

“Tumeituma huko muda mchache uliopita. Tunaamini saa 10 jioni au 11 kwa saa za Afrika Mashariki watakuwa na uhakika.

“Wakiipokea, maana yake anaweza kuanza kuitumikia timu yake mpya,” alisema ofisa huyo.

Alipoulizwa Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda alisema watalizungumzia suala hilo.


“Bado ni suala linaloshughulikiwa. Tunaweza kupata uhakika wake baadaye kidogo halafu tutalizungumzia,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV