June 23, 2016

Mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya Bin Slum Tyres, Mohammed Bin Slum (katikati) akisaini mkataba pamoja na Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe (kushoto) na Meya wa jiji la Mbeya, David Polela.

Kampuni ya Binslum Tyre kupitia betri zake imara za magari za RB, leo Alhamisi imeongeza mkataba wa kuendelea kuidhamini timu ya Mbeya City kwa miaka mingine miwili mingine baada ya ule wa awali kumalizika.

Binslum kwa mara ya kwanza kupitia RB ambazo ni kwa ajili ya magari makubwa na madogo, iliingia mkataba na timu hiyo Juni, 2014 ambapo umemalizika mwezi huu, huku huu wa sasa ambao una thamani ya shilingi milioni 300, ukitarajiwa kumalizika Juni, 2018.

Katika hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika kwenye ofisi ndogo za kampuni hiyo zilizopo Kariakoo jijini Dar, mbali na waandishi wa habari, pia ilihudhuriwa na Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Polela Mwashilindi na Makamu Mwenyekiti wa Binslum, Mohammed Binslum.



 Binslum amesema: “Tumeona tuna kila sababu za kuendelea kuidhamini tena Mbeya City kwa miaka mingine miwili baada ya kuonekana ni mabalozi wazuri wa bidhaa zetu.

“Kwenye mkataba wa awali walifuata kile ambacho tulitaka wakifanye, hivyo hatukuwa na maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kuongeza mkataba. Mkataba huu mpya una thamani ya shilingi milioni 300.”



Naye Kimbe alisema wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa kampuni hiyo katika kuzitangaza bishaa zao na wanaishukuru kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote cha mkataba wa awali na wanaamini itakuwa hivyo kwa mkataba huu mpya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic