June 8, 2016


Huku gumzo la kwamba anakwenda Yanga, Oman au anabaki Azam FC likiendelea, mshambuliaji nyota wa Azam FC, Kipre Tchetche ameamua kwenda Dubai kula bata.

Kipre raia wa Ivory Coast ameonekana ‘akila maisha’ na mkewe Prisca pamoja na kijana mmoja katika moja ya hoteli za kifahari za Dubai.

Tayari Azam FC ilishatoa ufafanuzi kwamba Kipre ni mali yake, lakini inaonekana Yanga imekuwa ikitamani kumjumuisha kwenye safu yake.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV