June 4, 2016Manchester United sasa wamepania kurejesha heshima yao baada ya kuwasilisha maombi kwenye klabu ya Barcelona kumtaka kumsajili Lionel Messi.

Klabu hiyo maarufu duniani, inataka kurejesha heshima na kucheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ilivyokuwa katika enzi za Alex Ferguson.

Imeelezwa Messi hana raha Hispania baada ya kuandamwa na kesi za masuala ya kodi. Kesi hizo bado zinaendelea.

Manchester United imewasilisha mara mbili ndani ya wiki tatu maombi ya kumtaka Messi.

Kama itafanikiwa bado italipa kiasi kikubwa cha uhamisho kuliko kile Real Madrid walicholipa kumpata Gareth Bale kutoka Tottenham.


Man United tayari imemnasa Kocha maarufu Jose Mourinho ikionekana ni sehemu ya kutaka kurejesha heshima yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV