June 4, 2016


Sasa ni uhakika Tanzania haina nafasi  ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa.

Mohamed Salah anayekipiga AS Roma, ndiye aliyefunga mabao yote mawili akianza na lile la kipindi cha kwanza la mkwaju wa adhabu baada ya beki Haji Mwinyi kufanya madhambi.

Kipindi cha pili, Mwinyi tena alifanya kosa kwa kuzidiwa nguvu na Salah akapachika bao la pili akiwa amtulia kabisa.


Salah alifunga mabao yake katika dakika ya 44 na 58 na kuikatisha tamaa kabisa Stars na mashabiki wengi waliojitokeza kuishangilia timu yao ya taifa.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alikosa penalti baada ya Himid Mao kuangushwa ndani ya enero la hatari.


Ushindi huo unaifanya Misri kufuzu baada ya kuwa imefikisha pointi 10, Nigeria iko katika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu na Tanzania inabaki mkiani na pointi moja.

Stars walicheza vizuri hasa kwa upande wa kumiliki mpira lakini tatizo likaonekana kutokuwa na mipango ya uhakika ili kujenga mbinu za kupata bao.

1 COMMENTS:

  1. Kwa mujibu wa mheshimiwa Rais,wachezaji wetu nao ni vilaza wa soka.Hawana jipya,tunachoweza kama Taifa ni fitina na majungu tu,hatuwezi jambo lolote katika uhalisia wake.Labda FIFA iruhusu wachezaji wa kigeni kwa timu za Taifa ndiyo walau tunaweza kutoboa,lakini kwa kutumia wachezaji hawa vilaza wa soka,hatuwezi kufika popote.Huoni yanga wachezaji wa kigeni wamewafanya wafike mbali?wenyewe hatuwezi chochote,sisi ni vilaza wa kila kitu.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV