June 10, 2016


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga ambaye anamaliza muda wake amewaomba wanachama wa klabu hiyo kumpa kura tena ili aweze kuendeleza alichokianza.

Sanga anagombea nafasi hiyo akichuana na Titus Osoro, hata hivyo, inaonekana wazi ataibuka na ushindi wa kishindo.

Hii inatokana na kazi nzuri aliyoifanya akishirikiana vizuri na Mwenyekiti, Yusuf Manji na kamati ya utendaji na kuifanya Yanga kuwa imara na yenye mafanikio.

Sanga ambaye si mzungumzaji sana, katika kipindi cha kupiga kampeni mbele ya wanachama wa Yanga kwenye makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam, alisema: 

“Mambo tuliyofanya ni ushahidi tosha, nichagueni mimi na Manji tuendeleze haya mafanikio tuliyopata, kumbukeni kazi ya makamu ni kufanya mambo anayoelekezwa na mwenyekiti au kuyafanya anapokuwa nje ya klabu au hayupo, ninaamini nimekuwa nikiyafanya kwa weledi mkubwa.”

Katika uchaguzi huo utakaofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar, jumla ya wagombea 20 wanawania nafasi ya ujumbe wa kamati kuu ambapo wanahitajika nane tu.


Miongoni mwao ni, Ayoub Nyenzi, Lameck Nyambaya, David Ruhago, Salum Mkemi, Samuel Lukumy, Tobias Lingalangala, Beda Tindwa, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ na Hussein Nyika.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV