June 18, 2016

WAMBURA

Michael Richard Wambura ameshinda na kuwa mwenyekiti mpya wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara.

Wambura ameshinda uchaguzi huo leo baada ya kubeba kura 26 kati ya 27 baada ya kuwa mgombea pekee na kupigiwa kura moja tu ya hapana.

Unaweza kusema ni ushindi wa kishindi na Wambura aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF, Kaimu Mwenyekiti wa Simba na hivi kugombea nafasi ya urais Simba akashindwa na Evans Aveva, sasa ni mwenyekiti wa chama hicho cha Mara.


Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Mara, leo, Wambura amesema: “Mimi ni mtumishi wa watu, tunatakiwa kupambana kuwasaidia Watanzania. Mimi ni familia ya mpira, vizuri nikaipigania kwa ajili ya kuleta maendeleo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV