June 18, 2016Uongozi wa Yanga uko katika pilika nenda rudi katika kuhakikisha inafanikisha zoezi la kumpa nafasi beki wake Hassan Kessy anacheza mechi ya kesho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Yanga iko Algeria tayari kuivaa Mo Bejaia katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, kesho. Kessy anakuwa tegemeo kwa kuwa beki Juma Abdul ni majeruhi.

Lakini, Shirikisho la Soka Afrika (Caf), tayari limeweka msisitizo kwamba Kessy na wachezaji wengine waliosajiliwa Yanga kama Andrew Vicent ‘Dante’ kutoka Mtibwa Sugar, Juma Mahadhi (Coastal Union) na Beno Kakolaki (Prisons) wanatakiwa kuwa na barua ya “kuwaachia”.

Viongozi wa Yanga, jioni ya leo ndiyo walianza pilika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa mara moja ili Kessy acheze mechi hiyo.

Tayari Kocha, Hans van der Pluijm ameweka wazi kwamba anamhitaji Kessy kucheza katika mechi hiyo.

Iwapo Simba, Mtibwa, Coastal Union na Prisons wataandika barua ya "kuwaachia" wachezaji hao, kila kitu kitakuwa laini kwa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV