July 8, 2016

YUSIF (KULIA) AKIFANYIWA MAHOJIANO NA WAANDISHI WA GAZETI LA CHAMPIONI.

Azam FC imeonyesha safari hii haitaki masihara, hii ni baada ya kushusha vifaa kutoka Ivory Coast, Hispania, Cameroon na Ghana na kutangaza kuwa na bado wengine wataingia muda wowote.

Lakini Mghana, Nurdeen Yusif ambaye ni beki wa kushoto ameonekana kuwa moto ambapo alikuwa ni mchezaji wa Medeama ya Ghana itakayotua nchini wiki ijayo kukipiga na Yanga katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Yusif alitua juzi usiku akitokea Ghana ambapo mchongo mzima ulisukwa na wakala aliyezoeleka Jangwani, Gibby ‘Rasta’.

Gibby ndiye aliyewaleta nchini nyota kadhaa wakiwemo Kipah Sherman, Vincent Bossou, Bobacar Issoufor Garba, Joseph Zuttah waliotua Yanga.

Yusif ambaye tayari ameanza mazoezi amezungumza na gazeti hili na kusema yeye bado ni mali ya Medeama, ana mkataba wa miaka miwili lakini amekuja Tanzania ili kutafuta changamoto nje ya Ghana.

“Nipo hapa kwa majaribio kuna mambo kati yetu hayajakaa sawa na nisipendi kuyazungumzia lakini wao walikuwa wakigoma kuniachia, ilifika sehemu nikaamua kuwagomea na nilipopata fursa hii ndiyo nikaitumia,” alisema Yusif.

Kuhusu Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, Yusif alisema: “Ni kocha anayejulikana kwetu, aliwahi kuifundisha Medeama lakini bahati mbaya mimi sikuwepo, nilikuwa kwa mkopo  nchini Moldova.” 


Mbali na Yusif, wageni wengine walio majaribioni kikosini hapo ni makipa Juan Jesus Gonzalez kutoka Tenerife ya Hispania na Daniel Yeboah wa Ivory Coast.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV