July 1, 2016


MURO
KAMATI YA MAADILI
Kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa ambazo zinaeleza kwamba viongozi wawili wa soka nchini watafungiwa kesho.

Inaelezwa kuna mpango huo ambao unalenga kuendeleza ubabe wa TFF kama ulimtokea Dk Damas Ndumbaro aliyekuwa akizitete klabu.

Mwingine anayeonekana anaweza kukutana na panga ni Nassib Mabrouk - Katibu wa MZFA na Msimamizi msaidizi wa kituo cha Mwanza.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  inatarajiwa kuwa na kikao chake Jumamosi Julai 2, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za TFF zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, makutano ya barabara za Shaurimoyo na Uhuru, Ilala jijini Dar es Salaam.

Viongozi watatu kutoka wanachama wa TFF wanahitajika kufika kwenye kikao hicho kinachotarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi.


  1. Viongozi hao ni Jerry Muro - Msemaji wa Young Africans S.C
  2. Nassib Mabrouk - Katibu wa MZFA na Msimamizi msaidizi wa kituo cha Mwanza
  3. Mbasha Matutu - Mjumbe wa mkutano mkuu Mkoa wa Shinyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV