July 4, 2016


Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema bado upo katika harakati za kuhakikisha unamnasa beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwa kuwa ndiyo chaguo lao.

Tshabalala ambaye msimu ujao atatambulika kama Zimbwe Jr, alitua Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kagera Sugar ambapo kwa sasa amekuwa lulu ndani ya timu hiyo kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa.

Mmoja wa mabosi wa Yanga amesema kuwa wapo katika harakati za kuhakikisha wanamnasa beki huyo kwa ajili ya kuleta changamoto kwa Mwinyi Haji na Oscar Joshua kutokana na viwango vyao kuonekana kupwaya.

Bosi huyo alisema kwa upande wao nafasi iliyobaki katika usajili wa msimu huu ni beki wa kushoto na kiungo mmoja ambao wataweza kuwasaidia katika ligi na mashindano ya kimataifa.

“Tunataka beki wa kushoto na chaguo letu ni Tshabalala wa Simba, huyo ndiyo atakuwa mtu sahihi wa kuweza kutoa changamoto kwa (Oscar) Joshua na (Haji) Mwinyi.

“Unajua tatizo halipo kwa mchezaji kwa sababu tumeshakutana naye zaidi ya mara nne na ameonyesha kukubali isipokuwa Simba ndiyo wanaonekana kuwa ni wagumu kwa kuwa bado wanamkataba naye wa mwaka mmoja,” alisema bosi huyo.

Alipotafutwa  Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Murro alisema kuwa kwa sasa hawezi kuliongelea suala hilo kwa kuwa bado halijafika mezani kwake.


Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni uongozi wa Simba uliwahi kusema hauna mpango wa kumuuza mchezaji huyo kutokana na kuwa ni msaada mkubwa ndani ya timu hiyo.

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Hivi kanuni za ligi zinasemaje kwa timu moja kuzungumza na mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine

    ReplyDelete
    Replies
    1. navyojua mm mchezaji anaruhusiwa kuongea na klabu nyingine ikiwa ktk mkataba wake amebakiza miezi 6 vinginevyo ni kosa

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV