July 19, 2016


HANS VAN DER PLUIJM, KOCHA RAIA WA UHOLANZI ALIYEIBEBESHA YANGA KOMBE LA LIGI KUU BARA NA KOMBE LA SHIRIKISHO MSIMU WA 2015-16.

Makocha wa kigeni watakaotaka kufundisha Ligi Kuu Bara, watakaguliwa na watalaamu wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Uamuzi huo umepitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo limesisitiza kuwa kwa makocha wakuu wa Ligi Kuu Bara ni lazima kuwa na Leseni A.

“Kwa kuwa makocha wa nyumbani watatakiwa kuwa na Leseni A, basi wale wa nje vyeti vyao vitatumwa Caf ambao watadhibitisha au kukataa.

“Hivyo kama timu inataka kuajiri kocha wa kigeni, lazima atume vitu vyake ili tuvitume Caf kwa ajili ya uthibitisho,” alisema Rais wa TFF, Jamal Malinzi.


Msimu ujao ndiyo utakuwa wa kwanza, kila kocha mkuu kulazimika kuwa na Leseni A.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic