July 18, 2016


TP Mazembe imejiongezea pointi moja baada ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya wenyeji wake Mo Bejaia katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

TP Mazembe walikuwa wageni wa Bejaia katika mechi ngumu usiku wa kuamkia leo na watakuwa na furaha baada ya kupata pointi hiyo moja muhimu.

Sare hiyo imeihakikishia TP Mazembe kufuzu hatua ya nusu fainali kwa asilimia 90 kwa kuwa kama itashinda mechi moja katika mechi tatu zilizobaki basi itakuwa ina uhakika wa asilimia 100.

Lakini sare hiyo, imezidi kudidimiza matumaini ya Yanga kuamka angalau na kupata pointi zitakazoiwezesha kubadili mambo kwa kuwa ina pointi moja tu baada ya kucheza mechi tatu ikipoteza mbili na kupata sare moja tu dhidi ya Medeama.


TP Mazembe inaendelea kuongoza kundi hilo ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Bejaia yenye tano, Medeama ina mbili na Yanga inaburuza mkia na pointi hiyo moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV