July 18, 2016
Na Saleh Ally
RAHA ya soka ni ushabiki, hakuna anayeweza kushangaa ndiyo maana mashabiki wa Simba wanaonekana kuwa na furaha sana kuona Yanga inafeli au kushindwa kusonga katika hatua ya Kombe la Shirikisho.

Yanga ndiyo wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho lakini kwa mambo yalivyo, hakika nafasi ya Yanga ni finyu na kama itabadilika, basi itakuwa ni ile miujiza ya kisoka.

Mashabiki wa Simba na timu nyingine, inawezekana Azam FC na nyinginezo wanaweza kuwa na furaha sana kwa kuona Yanga inafeli. Maana sasa katika Kundi A inaendelea kushika mkia baada ya sare moja katika mechi tatu.

Sare hiyo inaifanya Yanga kuwa mkiani ikiwa na pointi moja tu, Medeama ya Ghana wanafuatia wakiwa na pointi mbili baada ya sare mbili na Mo Bejaia na TP Mazembe hata kabla ya mechi ya jana na baada ya mechi hiyo, watabaki kwenye nafasi ya kwanza na ya pili.

Mashabiki hasa wa Simba, waliishangilia sana Medeama, hata mashabiki wa Yanga wangeweza kufanya hivyo kwa Simba kama ingekuwa hatua hii, au waliwahi kufanya hivyo, mfano wakati Simba ikichapwa na TP Mazembe miaka michache iliyopita.

Mimi ni mtumishi wa wapenda michezo, sioni vibaya kuwashawishi wasomaji wa gazeti hili kwamba bado suala la uzalendo linapaswa kupewa kipaumbele kama utalinganisha na kila kitu. Yanga ni ya Tanzania na si kutoka Ghana, DR Congo au Morocco.

Mashabiki kwangu pia wanaweza kuwa si tatizo sana lakini ningependa kutupa jicho mbali sana hasa kwa viongozi wa klabu nyingine ambao wanaonekana hawajitambui na wanajiona wao ni sehemu ya mashabiki wa soka.

Si sahihi kiongozi wa klabu kubwa kuonyesha ushabiki kama ule unaoweza kuonyeshwa na shabiki wa kawaida wa soka aliye jukwaani. Nasema hivi kwa kuwa mmoja wa viongozi wa klabu maarufu nchini, alionekana kuchanganyikiwa baada ya Medeama kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga.

Kiongozi huyo alikuwa na furaha, jasho linamtoka na hata akafikia kuwapongeza wachezaji wa Medeama baada ya mechi dhidi ya Yanga, juzi Jumamosi. Kwamba amefurahishwa na sare hiyo.

Angeweza kufurahi kama shabiki, lakini kama kiongozi pia anapaswa kujiuliza klabu ambayo anaiongoza imefikia wapi? Iko wapi na mafanikio yake yakoje kwa kipindi husika.

Inawezekana presha yake kubwa ilianza baada ya Yanga kubwa bingwa Tanzania Bara, ikaendelea ilipokuwa bingwa Kombe la FA. Huenda imemkera zaidi ilipofikia kucheza Kombe la Shirikisho. Kwake ilikuwa si vema Yanga ikafanikiwa.

Ushabiki wake unaweza usiwe hoja ya msingi au tija, hoja kuu linaweza kuwa swali la kipi alichokifanya kuisaidia timu au klabu yake kupata maendeleo makubwa?

Huyu anayefurahia timu nyingine kufeli, huku yake ikiwa haina hata mfano wa mafanikio, anapaswa kuwa kiongozi? Binafsi ninaingiwa na hofu kwa kuwa kiongozi bora alipaswa kuwa na malengo, anayepaswa kujifunza na anayetaka kutimiza ndoto.

Kiongozi anayefurahia Yanga iishie njiani, yeye timu yake ameiandaa? Alipaswa kufurahia au kujifunza zaidi? Kweli alipaswa kuonyesha amechanganyikiwa kwa furaha kuona Yanga imetoka sare?

Kama anapata muda huo, wakati gani anapata muda wa kufanya maandalizi ya kutosha na kuisaidia klabu yake? Jiulize kiongozi kama huyo ambaye yeye ameishafeli kwa misimu kadhaa. Kweli anapaswa kuwa na furaha kuona wengine wanafeli pia?


Maana yake amekubali kufeli kwake na angefurahi wengine wafeli zaidi kwa kuwa yake ipo taabani na haifanyi vizuri. Sasa maendeleo ya soka yanatokea wapi? Ushauri wangu ni hivi, ushabiki hauepukiki lakini vizuri kuwa na staha katika hili kuepuka kuonyesha upungufu wako hadharani bila ya kujua unajimaliza.

8 COMMENTS:

 1. Tatizo lako unazi umekuwa mwingi sana kuliko weledi wa kazi yako.Ni mara ngapi Jerry Muro ametumia Lugha za kuudhi dhidi ya viongozi wa timu pinzani?Anavyowaita wenzake "wa matopeni" hiyo ni lugha ya kimichezo?Badala ya kugeuka na kuanza kushusha lawama kwa watu wasiohusika,iambie timu yako idhihirishe "ukimataifa wake" dimbani,badala ya kuibeba magazetini.Kiongozi unayemsemea hapa hata angeshangilia akiwa mtupu,bado asingeweza kuyabadili matokeo ya uwanjani,jambo la msingi ni timu zetu ziache figisu namipango ya ushindi ya nje ya uwanja.Zicheze mpira na bingwa apatikane kutokana na uwezo wake uwanjani,na si uwezo wa mfuko wake.Ona mnavyoaibika uwanjani kutokana na kuupata ubingwa kimagumashi.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Umenikosa sana Bother kwa maoni yako mazuri isingefikia hatua hii ya mashabiki kuishangilia timu pinzani kwa kiasi hiki kama si Jery muro ambaye amekuwa mstari wa mbele kuiponda simba kuliko kukosoa mapungufu ya timu yake!! mbona zipo timu nyingi tu za nje ambazo hazina mafanikio kwa muda mrefu mbona hatujawah kusikia wasemaji wa klabu wakiongea vijembe na maneno mabovu kama ya muro? Saleh jembe unapaswa kujitathmin kabla ya kuleta maoni yako mbele ya wadau la sivyo utakuwa upunguza heshima yako iliyojengeka kwa wadau wa soka

   Delete
 2. unaandika kishabiki sana makala zako kwani nani asiyejua kuwa ww ni yanga wa kutupwa? huyo kiongozi aliingia uwanjani kama kiongozi au shabiki wa kutazama mpira? kwani hao yanga wangeshinda unadhani wangewatambia nan? madema au simba? et kafanya nn kuisaidia timu yake kwani huko kuchanganyikiwa unakokuita ndyo atachanganyikiwa mwaka mzima bila kufanya kazi zingine? au ww ulitaka hakacrike? simba ikifungwa viongizi hadi mashabiki wa yanga wanafurah na yanga vile vile punguza ushabiki kuandika vitu visivyo na maana wala tija kwenye soka

  ReplyDelete
 3. Ukweli unauma, mtaumia sana. Poleni na mjipe moyo.

  ReplyDelete
 4. Nyie wa matopeni tu,andaaeni timu kwa kudra za mwenyezi mungu nanyi mshiriki 2018 km sio 2019,hao mnaowazomea bd in wawakilshi wenu ht mwakani
  Sasa mapovu yanawatoka nini wkt mwandishi anawakumbusha viongozi wenu mazombi wale watengeneze timu km kununua ili mradi duka mnalijua kanunueni nanyi,ile ndo ya kimataifa,we angalia zawadi za vpl nazo wamenunua? Acheni hz figisu zenu

  ReplyDelete
 5. Mwakani Yanga na Azam wapo kimataifa. Labda, narudia, labda mwaka kesho kutwa ndiyo wamatopeni wanaweza kushiriki kimataifa. Huyo kiongozi aelekeze nguvu zake huko. Kwanza afurahi angalau ameweza kuangalia mechi ya kimataifa. Ingekuwa Yanga haishiriki, angefanya nini? Arudi klabuni kwake wakaendelee kusajili wachezaji na kumpa kocha. Baadaye ligi ikianza waendelee kumpangia timu ili Yanga na Azam wazidi kupeta.

  ReplyDelete
 6. Msomi huaongea na uandika kisomi zaidi! Usinishangae ila nikubali ikibidi nichukie...haya makala ni ya kiusomi au? Mimi sijui! Wanasaikolojia hatushangai hili....ilia ni ukosefu wa uelewa juu ya saikilolojia ya wanadamu. Kiasili binadamu huwa na tamaa ya kufanikiwa na pengine huwa na furaha zaidi paleanapoona anafanikiwa na wenginegine wako chini yake, na huchukia zaidi kuona nazidiwa na wengine na hapo huanza juhudi za kuwashusha wengine...Kimsingi, hakuna mtu ambaye hufurahia mafanikio ya mingine. Suala la kiongzozi wa timu kuishangilia timu nyingine si jambo la kushangaa, bali ni la kushangaa kwa wale ambao hufikikiriwa na wengine. Hata ingelikuwa ni Yanga hawashiriki, bado viongozi wao wasingelihuzunika kuona timu nyingine zinafanya vizuri. Kiongozi ni binadamu kama binadamu mwingine. Ni ushamba wa hali ya juu kusema ati mashindano ya vilabu ya CAF yanakuwa na yanawakilisha nchi.... hakuna bali ni vilabu vyenyewe ndivyo vinajiwakilisha, hakuna dhana ya uzalendo hata siku moja, uzalendo ni kwa mashabiki ni pale bendera ya taifa inaposimamishwa kwa timu ya taifa maana pale ianakuwa ni wachezaji wa kitanzania, vilabu si nembo ya taifa na ndio maana hata nyimbo za taifa hazipigwi pale. Mpira wa soka ni mtu kufurahia upande anaoona unamvutia na si vnginevyo. Halafu dhana ya kwamba sijui Yanga wamefanikiwa,,, ni kujiziba macho, wamefanikiwa kwa lipi? VPL na FA ambazo zimeendeshwa kimagumashi...upuuzi kwa kujisifia kwa hili. Mafanikio yao wayaoneshe kimataifa. Ni ujinga wa kiwango cha PhD....Wamecheza CAF champions league wmefail wakaenda Shirikisho hala tunasema wamefanikiwa kwa kiwango kipi? Ukitaka kujipima kuwa umefanikiwa jilinganishe na wenzako ktk hilo unalofanya walifikia wapi? Mwaka 2003,ingekuwa km sasa hivi Simba si wangecheza pia Shirikisho? Lakini sheria hiyo haikuwepo.Lakini bado ktk CAF champions league Simba walipata points ngapi? Hawa wana 1 hadi sasa halafumnasema wamefanikiwa, huu ni ushamba na ushabiki wa kijinga. Kwa bongo hatupaswi kuchekana ktk mechiz za kimataifa.

  ReplyDelete
 7. Nadhani mwandishi pamoja na mashabiki wenzie hawaelewi kwamba sasa umefika wakati wa kuvuna kile walichokipanda katika VPL na kombe la shirikisho. wao walidhani marefa wa CAF watakuwa wale wenye kutumikia pesa za mwenyekigoda? hayo ni madhara ya kushadadia timu kubebwa na mkiona tunafurahia ni kuwajenga katika misingi ya kuwafanya muachane na mfumo wenu wa ushindi kimagumashi. hata hiyo point moja ni uzembe tu wa hao madeama wala hamkustahili kuipata na tutawacheka sana. mmezoea kubebwa bebwenina huko basi.

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV