Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ametoa onyo kali kwa wanaoshiriki masuala ya rushwa michezoni na hasa kwenye soka.
Mwigulu ambaye ni kati ya mastraika wa timu ya Bunge amesema amekuwa akishangazwa na ujasiri wa watu ambao wako tayari kutoa rushwa hata kwenye timu za polisi au jeshi.
“Kweli unatoa rushwa kwa timu ya Mageraza ili ifungwe, unatoa rushwa kwenye timu ya Polisi au Jeshi. Ujasiri wa namna hiyo unautoa wapi.
“Natoa angalizo na onyo kwamba sisi tutalishughulikia hili na waliokuwa wakishiriki waache mara moja,” alisema Mwigulu ambaye ni Mgeni Rasmi katika utoaji tuzo katika hafla ya wachezaji bora na washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom usiku huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment