July 5, 2016


 Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama ya Ghana.

Mazoezi ya Yanga kama ilivyokuwa jana, yamefanyika kwenye Uwanja wa boko Veterani jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm akisaidiwa na Juma Mwambusi na Juma Pondamali.

Leo kidogo ilikuwa tofauti, wachezaji wa Yanga walifanya mazoezi ya kasi na baadaye kucheza mpira.

Mazoezi yao yalionyesha kuwa ni yale ya kweli kwa kuwa watu hawakutaka utani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV