July 2, 2016

CHIRWA
Baadhi ya mashabiki wakiwemo watu mashuhuri Yanga wamelaumu uwezo wa straika wao mpya, Obrey Chirwa lakini kocha wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm amesema watulie mchezaji huyo ataonyesha makali hivi karibuni.

Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, ndiye alimtupia lawama Chirwa baada ya mechi ya TP Mazembe huku akilalama fedha nyingi zimetumika kumsajili ingawa hakusema fedha hizo zimetokea wapi.

Chirwa aliyesajiliwa na Yanga hivi karibuni kutoka FC Platinum ya Zimbabwe, Jumanne wiki hii alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya TP Mazembe ambayo ni ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

PLUIJM
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga ilifungwa bao 1-0.

Pluijm amesema:
“Kwa siku nne ambazo tumekuwa naye, naweza kusema Chirwa ni moja ya washambuliaji bora, anaonekana ni straika mwenye akili ya mpira, jinsi anavyomiliki na kukimbia na mpira.

“Chirwa anatakiwa kufanya mazoezi nasi ili kuendana na mfumo wa timu, lakini pa kuanzia Chirwa ni mchezaji bora na akizoea zaidi wenyewe watamfurahia,” alisema Pluijm.

Yanga inaendelea na mazoezi yake jijini Dar es Salaam na baada ya Sikukuu Idd El Fitri itaweka kambi Zanzibar.

SOURCE: CHAMPIONI  

1 COMMENTS:

  1. Tuliambiwa Isaffou boubakar kuwa anazoea mazingira hadi akatimuliwa,sasa na huyo Chirwa mambo ni hayohayo!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV