July 2, 2016


Dakika chache tu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuinoa Simba, Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon amesema anataka kusajili mastraika wawili na mabeki wawili wa kati wa kigeni ili kuiongezea nguvu timu yake.

Tayari uongozi wa Simba umeshafanyia kazi ombi hilo na imeshamalizana na straika wa Vital’O ya Burundi, Laudit Mavugo ambaye amemaliza mkataba kwenye timu yake. 

Mmoja wa mabosi wa Kamati ya Usajili ya Simba, alisema, Omog amependekeza usajili huo ili kuifanya timu iwe na nguvu ya kupambana msimu ujao.

“Kocha ametoa mapendekezo ya baadhi ya nafasi ambazo lazima usajili wake uwe mkubwa ili kuleta chachu ya ushindi kwa kila mechi tutakayoicheza ya ligi kuu au michuano mingine.

“Moja ya sehemu ambazo alihitaji zifanyiwe marekebisho ya usajili ni safu ya ushambuliaji na ulinzi ambayo kila sehemu anahitaji wachezaji wawili wa kigeni watakaokidhi vigezo vyake.” 

Alipotafutwa Rais wa Simba, Evans Aveva alisema: “Awali tulifanya usajili wenyewe, lakini baada ya kocha kutua tumepanga kukutana naye ili kujadili mambo ya usajili, haina tatizo.”0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV