July 5, 2016


Beki tegemeo wa Chris Smalling ameumia vibaya kwa kupasuka juu ya jicho baada ya kuanguka ghafla na kujigonga.

Kidonda chake kimeelezwa ukubwa wa inchi tatu na kulazimika kushonwa nyuzi kadhaa wakati akiwa katika mapumziko katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia.

Inaelezwa beki huyo alianguka baada ya kula chakula chenye chembechembe ambazo huenda kuwa zinatokana na samaki au mbogamboga ambazo si zile zinazwekwa kwa makusudi.

Beki huyo tegemeo Man United na England tayari ameishapatiwa matibabu na anaendelea vizuri.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV