August 19, 2016

Simba ilikuwa ikimsubiri kwa hamu kipa wa Azam FC, Mwadini Ali ambaye ilielezwa angekwenda kwa mkopo, sambamba na fowadi, Ame Ally ‘Zungu’, hata hivyo dili la Mwadini liliyeyuka ghafla na sasa kipa huyo anadunda ndani ya Azam.

  
Hata hivyo, imebainika kuwa chanzo kikuu cha kugeuzia gia angani ni kipa Muivory Coast, Daniel Yeboah ambaye walikatisha mpango wa kumsajili mwishoni kabisa mwa usajili na kuamua kuimarisha zaidi safu za ndani hivyo kubatilisha mpango wa kumtoa Mwadini.

Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba amekiri kuwa mpango wa kumtoa kipa huyo kwa mkopo ulikuwepo wakati Ame anatua Msimbazi lakini wakabadili maamuzi ghafla, hivyo Muivory Coast kuachwa yeye pamoja na Mhispania, Gonzalez Jesus waliyokuja majaribioni.

“Kweli Mwadini alikuwa aende Simba lakini baadaye tuliamua kumbakisha na akachukua nafasi ya Daniel ambaye tuliachana naye ili tuimarishe zaidi nafasi za ndani katika usajili wa wachezaji wa kigeni,” alisema Kawemba.

Nyota wapya wa kikosi hicho ni Frasicsco Zekumbariwa (Ivory Coast), Daniel Amoah (Ghana), Golanzo Ronardo (Ivory Coast), Bruce Kangwa (Zimbabwe) na Enock Agyei (Ghana-aliyeachwa kwa mkopo Medeama). Wanaungana na Kipre Bolou (Ivory Coast), Jean Mugiraneza (Rwanda) na Pascal Wawa (Ivory Coast).




SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV