August 22, 2016

Kufuatia taarifa kuwa klabu kadhaa zinamuwania beki wa Manchester United, Phil Jones imefahamika kuwa kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho hataki kumuuza kwa kuwa bado yupo katika mipango yake.
  

Klabu kadhaa zikiwemo Stoke City, Watford, Hull City na Arsenal zimetajwa kuwa miongoni mwa zinazomuwania mchezaji huyo ambaye inaonekana amekosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.


Mourinho bado anamhitaji mchezaji huyo katika mechi zijazo ambapo anajua kutakuwa na ratiba ngumu dhidi yao, ndiyo maana hataki kumruhusu kuondoka.
  


 Tayari United imemruhusu beki wake chipukizi, Cameron Borthwick-Jackson kwenda Wolves kwa mkopo lakini upande wa Jones ambaye ni ‘bingwa wa kuumi’ kutokana na staili yake ya kucheza kwa kutuma nguvu bado anaweza kuendelea kubaki klabuni hapo japokuwa lolote linaweza kutokea.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV