Mshambuliaji mpya wa Juventus, Gonzalo Higuain amewajibu wale wote wanaomuita yeye ni kibonge kuwa atawakosoa kauli zao hizo kwa kufanya kweli katika timu yake, akimaanisha kuwa anataka kufunga mabao mengi ili kuonyesha ubonge wake hauwezi kuathiri kipaji chake.
Straika huyo ambaye amesajiliwa hivi karibuni klabuni hapo kwa ada ya pauni milioni 78, iliripotiwa kuwa ameongezea uzito hali ambayo inaweza kuathiri kiwango chake licha ya kusajiliwa kwa dau kubwa lakini wikiendi ya jana alifanya kweli kwa kufunga bao la ushindi kwa Juventus katika mechi ya ufunguzi wa Serie A.
“Ni vizuri wakiendelea kusema kuwa mimi ni mnene, nitaendelea kufunga zaidi. Nimefanya mazoezi kwa siku 20 na ukweli ni kuwa sielewi hayo maneno yalikuwa yakitoka wapi,” alisema Higuain.
0 COMMENTS:
Post a Comment