August 28, 2016


Mashabiki wa JKT Ruvu waliojitokeza jana kuishangilia timu yao wakati ikicheza na Simba walionekana kuwa kivutio kikuu kwa mashabiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki hao walioelezwa kuwa ni askari au wanafunzi pia kikosi cha michezo cha JKT upande wa wanawake katika michezo, walikuwa wasichana warembo lakini wote wamenyoa ‘unga’ flani hivi.

Hali ilifanya baadhi ya mashabiki wa Yanga kuwaunga mkono wakati walipokuwa wakiizomea Simba au kuwashangilia wachezaji wao.

Mechi hiyo ya pili ya Ligi Kuu Bara kwa timu yao na Simba, iliisha kwa sare ya bila bao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV